Title Image

TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA TAIFA YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SITA NA DARASA LA NNE YA MWAKA 2017, JUMATATU TAREHE 29 JANUARI 2018.

news phpto

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma akitoa muhtasarai wa matokeo ya kidato cha pili, darasa la sita na darsa la nne kwa mwaka 2017

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma ametangaza matokeo ya kidato cha pili, darasa la sita na darasa la nne kwa mwaka 2017 ambapo matokeo hayo yameonesha kuongezeka ufaulu kwa asilimia 3.88 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2016. Akifafanua taarifa hio alisema jumla ya watahiniwa 34,458 sawa na asilimia 73.98 ya watahiniwa wote wamefaulu, kati yao wanawake ni 20,793 sawa na asilimia 60.34 na wanaume ni 13,665 sawa na asilimia 39.66. Ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.88 ukilinganisha na watahiniwa 17,581 sawa na asilimia 70.1 kwa mwaka 2016. Watahiniwa 12,122 hawakufaulu wakiwemo 5,789 wa Kidato cha Pili (6) na 6,333 wa Kidato cha Pili (7) sawa na asilimia 26.02. Tafadhali bofya HAPA KUPATA TAARIFA KAMILI