Title Image

NMB YATOA MSAADA KOMPYUTA 50 KUUNGA MKONO SEKTA YA ELIMU

news phpto

waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma akipokea msaada wa kompyuta 50 kutoka kwa Bi. INEKE BUSSEMAKER Mkurugenzi Mkuu wa NMB, mwanzo kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Aamali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma amewataka Wadau mbali mbali wa Elimu, yakiwemo Mashirika na Taasisi Binafsi kuendelea kuunga mkono sekta ya elimu kwa ajili kujenga mustakbali mwema wa vijana wetu na Taifa kwa ujumla.

Mhe. Riziki aliyasema hayo mara baada kupokea msaada wa kompyuta 50 kutoka Benki ya NMB kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Bi. Ineke Bussemaker katika hafla fupi iliyofanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali - Mazinzi Unguja.

Sambamba na hilo, Mhe. Riziki amewshukuru NMB kwa misaada yao wanayoitoa kwa sekta ya Elimu na kuwaahidi kuitunza na kuhakikisha inatumika kama ilivyo pangwa. Alieza kwamba kompyuta hizo zitapelekwa katika Skuli na Vituo vya Walimu ili kuongeza kasi ya kujifunza na kufundishia kupitia teknolojia hii ya TEHAMA.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker alifafanua kwamba Benki yake (NMB) inatenga kila mwaka asilima moja ya faida yake kwa ajili ya kuchangia shughuli za kijamii ikiwemo sekata ya elimu, afya na mambo mengine ya kijamii. Bi. INEKE alieleza kwamba NMB imetenga shiling 1.5 bilion ambazo zinagawanya katika Mikoa mbali mbali ya Tanzania ambako NMB inatoa huduma. Katika mwaka 2016 NMB ilichangia madawati 450 kwa ajili ya wanafunzi wa skuli mbali mbali za Zanzibar.