Title Image

SERIKALI YAKEMEA MATUMIZI MABAYA YA KOMPYUTA NA MITANDAO

Naibu Katibu Mkuu Taaluma Bi. Madina Mjaka Mwinyi akemea tabia ya baadhi ya walimu na watendaji wengine wa umma kuwa na matumizi mabaya ya kompyuta na vifaa vyengine vya TEHAMA. Ameeleza kuwa, lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuimarisha miundombinu ya TEHAMA katika skuli na ofisi za umma ni kuengeza ufanisi wa utendaji kazi pamoja na kuimarisha ubora wa elimu na si vyenginevyo. Hivyo amewaonya wale wote wenye tabia ya kugeuza malengo hayo kuacha mara moja tabia hiyo na badala yake wajikite katika maadili mazuri ya kazi zao.

Bi, Madina ameyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Elimu Ndugu Omar Said Ali alipokuwa akifungua mafunzo maalumu ya usimamizi wa mifumo ya TEHAMA na mtandao katika Skuli ya Sekondari Kwarara yaliyotolewa kwa Maafisa TEHAMA kutoka Wizara Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Maafisa kutoka Wizara Ujenzi Miundombinu na Usafirishaji.

Pia amesisitiza, Serikali imewekeza miundombinu mbali mbali ya tehama ikiwemo kuweka mkonga wa taifa na kuusambaza nchi nzima, imeimarisha huduma za mawsiliamo ya simu na kuongezeka vyombo vya habari vya TV na redio kila uchao ni jambo linatoa ishara njema kwa nchi yetu juu ya kukuwa sekta hii. Pia Serikali imeanzisha Idara mbali mbali za TEHAMA pamoja ile ya Serikali Mtandao na kutoa mafunzo kwa watendaji wake ili kuleta tija na kuhakikisha nchi yetu haiwachwi nyuma katika sekta hii sayansi na tekonolojia.

Hivyo ni matajio yetu mafunzo haya yakujengeeni uwezo wa utendaji na usimamizi bora wa mifumo na miundombinu ya tehama na hatimae nchi yetu iweze kufadika vizuri na fursa zilizomo katika sayansi na teknolojia.