HAFLA YA UFUNGUZI WA KITUO CHA MAANDALIZI TUTU MCHIKICHINI
Waziri wa Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar mhe. Lela Muhammed mussa amekutana na kufanya mazungumzo na watendaji wa idara ya mipango, Sera na utafiti wa wizara ya elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar, katika ukumbi wa mkutano wa wizara ya elimu Mazizini mkoa wa mjini magharibi unguja.
Katika kikao hicho Mambo mbalimbali ikiwemo mafanikio na changamoto zinoikumba idara hiyo.
Aidha katika kikao hicho alihudhuria na naibu waziri wa elimu Zanzibar mhe Khadija Salum Ali na Naibu
Katibu Mkuu utawala ndugu Amos John Henock.
Waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Mhe Lela Muhammed Mussa amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa chuo cha Victoria Institute huko ofisini kwake mazizin unguja.
Lengo la mazungumzo hayo ni kuendeleza mashirikiano katika sekta ya elimu nchini. Katika mazungumzo hayo alihudhuria na naibu katibu mkuu taaluma wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Dkt. Mwanakhamis Adam Ameir.
IMAGINE WORLDWIDE TANZANIA KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA MSINGITEK (KKK)