Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na wafanyakazi wote Leo tarehe 7/03/2024, wamesoma hitma ya kumuombea dua Aliye kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuanzia Mwaka 1964 hadi 1965 ambae pia ni Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Mzee Ali Hassan Mwinyi. iliyo fanyika katika Mskiti wa Jamii _Zej-Bar huko mazizini - Unguja.
ikiwa ni siku ya mwisho ya wiki moja ya maombolezi ya kifo chake , Wizara imesoma hitma hiyo kwa ajili ya kumuombea dua kutokana na mchango mkubwa na jitihada alizozifanya katika Wizara hiyo.
Imetolewa na kitengo cha Habari na Mawasiliano( WEMA).