Serikaali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kuchua hatua mbali mbali kuhakikisha waandishi wa habari wanafanyakazi katika mazingira mazuri ili kufikisha ujumbe kwa jamii na kuchochea maendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya Wziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh Lela Muhamed Mussa, Naibu Katibu Mkuu Utawala wa Wizara hiyo Ndg Khalid Masoud Waziri katika hafla ya kutunuku tunzo na vyeti kwa waandishi wa habari chipukizi wa SUZA amesema hatua hiyo inalenga kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa jamii na kuimarisha maendeleo nchini.
Amefahamisha kuwa teknolojia ya habari duniani inaendelea kukuwa kila siku hivyo ni vyema waandishi wa habari kuendelea kujifunza ili kuendana na mabadiliko hayo.
Nae Mkuu wa Skuli ya Habari na Mawasiliano SUZA Dk Ali Adnan amefahamisha kuwa lengo la kuandaa tunzo hizo ni kuhakikisha wanafunzi wanaotoka katika chuo hicho wanaendana na soko la ajira duniani.