SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar inatangaza nafasi za masomo zilizopokelewa kutoka ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania kwa ngazi za Shahada ya Kwanza, Uzamili na Uzamivu kwa mwaka wa masomo 2025/2026. (Turkiye Burslari-YTB).

Taarifa zaidi kuhusu vigezo vya muombaji (Admission Requirements), utaratibu wa maombi (Admission Procedures), fani za kujiunga (Programmes for Admission) na faida za ufadhili (Scholarship Benifits) zinapatikana katika tovuti: https://turkiyeburslari.gov.tr   

Mwisho wa kupokea maombi hayo tarehe 20 Febuari, 2025.

Muombaji anatakiwa atume nakala laini (soft copy) ya fomu ya maombi Pamoja na nakala ya vyeti vyake alivyomaliza masomo kupitia barua pepe zilizoainishwa hapo chini.

 

Imetolewa na:

Katibu Mkuu,

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,

S.L.P 394

Mazizini

Zanzibar.

Barua Pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.|This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.